Asili ya Athletics na olimpik | Michezo | DW | 24.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Asili ya Athletics na olimpik

Riadha au Athletics ndio moyo wa michezo yoyote ya olimpik tangu asilia.

Katika kalenda ya michezo ya Olimpik ya Beijing August,8 mwezi ujao hadi August 24,mchezo mmoja utakua kiini na shina la michezo mizima ya Olimpik:RIADHA au ATHLETICS.

Kwani, athletics ndio moyo na msisimko wa michezo yoyote ya olimpik,tena tangu mfaransa Pierre de Coubertin, alipoifufua michezo ya kwanza ya kisasa ya olimpik-modern Olympic Games- hapo 1896 mjini Athens,Ugiriki.

Ramadhan Ali leo an atusimulia juu ya riadha na olimpik na neno "Athletics" linatokana na neno gani la Kigiriki:

Neno "athletics"-riadha linatokana na asili ya neno la kigiriki "Athlos"-lenye maana vita au mapambano .Na huu ni mchezo au mashindano wa asili kabisa kama mwanadamu binafsi. Ni mashindano yanayojumuisha kukimbia,kuruka na kurusha.Ni mashindano ambayo yamegunduliwa yakifanyika katika ugiriki ya kali na hata kisiwani ireland.

Vitabu na maandishi ya kigiriki vikielezea mashindano ya mbio huko Hellas zaidi ya miaka 1000 kabla enzi za ukristu na michezo ya kale ya olimpik iliotangulia hii ya kisasa ilioanzia 1896 mjini Athens,ilishindaniwa kwanza huko Olympia-kaskazini-magharibi mwa Peloponnese.

Tarehe halisi zatafautina kuhusi lini hasa michezo ya kwanza ya kale ilifanyika.Mshindi wa kwanza ambae taarifa zake zinajulikana ni Coroebus hapo mwaka 884 BC. Coroebus alishinda mbio za stadion-mbio za masafa ya mita 200 na ndio mashindano pekee yaliokuwamo katika orodha ya michezo hiyo ya asilia.

Baadae wagiriki wakaanza kutimka mbio,wakachupa -long jump na kurusha kisahani -Discus na kurusha mkuki-javelin.

Na baada ya mfalme wa kirumi Theodosius alipopitisha sheria ya kuikomesha michezo ya Olympic ya asilia hapo mwaka 393 AD, mchezo wa athletics-riadha ulidumu na kushindaniwa katika mashindano ya wanajeshi hadi karne ya 19 pale msingi wa mashindano ya kisasa ya riadha ulipowekwa huko Uingereza enzi za malkia victoria.

Pale michezo ya kwanza kabisa ya kisasa ya olimpik-modern Olympic Games ilipofanyika Athens,1896,riadha-athletics- ulisalia kama mashnindano tulöioselelea nayo hadi leo.Na ndio shina la michezo ya kisasa ya olimpik kama tutakavyosisimka huko Beijing pale wanarioadha wa Afrika, wake kwa waume akina Kenenisa Bekele wa na Turnish Dibaba wa Ethiopia na Martin Lel na Janeth Chepkosgei wa Kenya, wakipepea bendera ya afrika wakifuata nyayo za marehemu Abebe Bikila .

mbio za kasi ni zile za masafamafupi ya mita 100-200 na 400-ambazo wanariadha wa Marekani na karibik wanatamba zaidi.

Mbio za masafa ya kati ni mita 800 na mita 1500 ambamo wanariadha wa Afrika hasa wa mashariki Kenya lakini pia Morocco hutia fora.Halafu kuna mbio za masafa marefu za mita 5,000 na 10.000-uwanja tena wa waafrika hasa wakenya na waethiopia.

Mbio ndefu kabisa za marathon zinachukua masafa ya km 42.195 na zina asili pia ya Ugiriki ya kale na mshindi wa kwanza kabisa wa mbio hizo PHIDIPPIDES aliekimbia kutoka mjio wa marathon hadi Athens,mji mkuu wa Ugiriki ili kutangaza ushindi wa wakaazi wa Athens dhidi ya waajemi kabla hakupinduka ghafula na kuaga dunia.

Michezo ya uwanjani isio ya kukimbia-yaani field events inajumuisha kuruka juu-high-jump,kuchupa -long jump na kuruka juu kwa upongoo pole vault.Mashindano ya kurusha katika sekta hii yanajumuisha kurusha mkuki,kurusha kisahani cha chuma na gololi la chuma-shot put.Michezo 10 mbali mbali kwa wanaume yanayomvika taji mwanariadha bora katika fani mbali mbali ya riadha ni decathlon-pia ni mchezo wenye asili ya kigiriki.Kwa wanawake ni pentahlon-michezo 7 mbali mbali.

Ulimwengu mzima basi kuanzia August 8 -24 mwezi ujao, utakodoa macho Beijing kuwaona wanariadha wake kwa waume wakinya n'ganayia medali za dhahabu,fedha na shaba katika medani ya riadha kama wenzao wsa Olimpia ya kale.