Amri ya kushambulia yatoka Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 09.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Amri ya kushambulia yatoka Pakistan

BERLIN:

Taarifa za vyombo vya habari vya Ujerumani zinasema kuwa wale washukiwa 3 wenye siasa kali za kiislamu waliokamatwa wiki iliopita kwa tuhuma za kupanga kuhujumu vituo vya Marekani nchini Ujerumani,wakifuata amri ya kikundi cha wafuasi wenye siasa kali nchini Pakistan.

Ripoti zinasema Umoja wa jihad wa kiislamu –Islamic jihad union-uliwaamuru vijana hao kufanya shmbulio hilo mwezi huu.

Njama ile ilizimwa jumaane iliopita pale polisi ilipowatia mbaroni wajerumani 2 waliosilmu na mturuki mmoja katika mkoa huu wa mto Rhine.

Washtaki wa serikali ya ujerumani wamesema vijana hao walijipatia vofaa vya kutengezea bomu lenye nguvu sawa nqa kilogramu 550 za TNT.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com