Algiers.Mabomu yaripuka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Algiers.Mabomu yaripuka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992.

Mabomu mawili mfululizo yameripuka nje ya vituo vya polisi karibu na mji mkuu Algeirs mapema leo asubuhi na kuuwa raia wawili na kuwajeruhi wengine 23 wengi wao wakiwa ni polisi.

Kwa mujibu wa maafisa nchini Algeria, hili ni shambulio la kwanza la mabomu katika nchi hiyo tangu pale kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2003.

Mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa kiislamu wa kundi la itikadi kali lijiitalo mahubiri na mapambano GSPC, linalaumiwa kwa kupoteza roho za watu kiasi cha laki mbili tangu mwaka 1992.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com