Al Hakim afariki dunia | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.08.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Al Hakim afariki dunia

Kongozi mkuu wa kiislamu wa kishia raq ameaga dunia Teheran.

Kiongozi wa mojawapo ya vikundi maarufu sana vya washia nchni raq, Abdulaziz al Hakim, amefariki katika hospitali ya Teheran,hii leo baada ya kupigana sana na maradhi ya kensa-hii ni kwa muujibu vyombo vya habari vya Iran vilvyoripoti.

Kiongozii huyu wa Baraza kuu la kislamu nchini Iraq ,alifariki muda mfupi baada ya kituo cha TV cha al -Furat kutangaza kwamba, Al-Hakim yuko taabani nchini Iran ambako akitibiwa kensa ya mapafu tangu miezii 4 iliopta.

Marehemu Al Hakim amekuwa Kiongozi wa Baraza la kislamu nchini Iraq tangu kuuwawa kwa kaka yake Mohamed Baqer al-Hakim katka mripuko wa bomu katika mji mtakatifu wa Najaf,kusini mwa Iraq, 2003.

Ukoo wake umeteseka sana hasa katika kipindi kirefu cha kinyanganyiro cha madaraka na amepoteza ndugu 6 kwa njama za kuuliwa kwa amri ya Saddam Hussein.Kwa kutwa korokoroni mara 3 kwa shughulii za uasi dhidi ya utawala huo enzi za Saddam Hussein,al-Hakim alikwenda Iran, 1980 kuishii uhamishoni.

Baraza kuu la kislamu nchin Iraq, lililoundwa mapema 1980,kwa msaada wa Iran, ni chama chenye nguvu kilichounda nguzo imara inayoegemea Umoja wa washiiia wa Iraq (UIA) unaotawala katika serikali ya muungano ya vikundi 20.

Baraza hilo ndilo kundi kubwa katika Bunge la Iraq wakat huu na lna usuhuba mwema na Marekani.Kwan, Al-Hakim alikua mjumbe wa Baraza la Iraq lilloteuliwa na Marekani baada ya kuvamiwa Iraq, 2003.Lakini kutokana na wadhifa wake wa kidini,hana wadhifa katka serikali ya Iraq.

Siku chache kabla hakuaga dunia,al-Hakm, aliehetiimu chuo kikuu maarufu cha kishia cha HAWAZ huko Najaf, alifaulu kuunda Umoja wa kitaifa wa Iraq -umoja mpya wa shikamano wa washia ulochukua nafasi ya ule uliokumbwa na mifarakano wa UIA kwea matayarisho ya uchaguzi wa Januari,mwaka huu.

Marehemu,aliekuwa na taba ya kuvuta sgara mno,mara ya kwanza kugunduliwa n a maradhi ya kensa ya mapavu hapo Mei, 2007 katika hospitali mjni Texas,Marekani.Akawa anatibwa mjiini Teheran halafu akarejea Baghdad, oktoba iiliofuata.

Mwanawe wa kiume Mohsen hakim aliwaamba maripota kwamba ukoo wao haungependa kifo kuripotiwa na vyombo vya habari na ungependa kuomboleza faraghani.Hatahvyo, inatarajiwa kwamba serikali ya Iran, iitamfanyia marehemu ibada maalumu ya kuomboleza katika chuo kikuu cha Teheran,kwavile aliishi kwa muda wa miaka 20 nchini Iran kabla kurejea Iraq,2003.

Mwandishi:Ramadhan Ali/DAPE

Mhariri:M.Abdul-Rahman

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com