Ahmedinejad asema ripoti ya upelelezi ni ushindi kwa Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 05.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ahmedinejad asema ripoti ya upelelezi ni ushindi kwa Iran

Rais wa Marekani George W.Bush ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Washington kuwa Iran bado ni tishio kwa amani duniani.Siku ya Jumatatu ripoti mpya ya upelelezi iliyotolewa na idara 16 za Marekani kuhusu Iran ilisema,Tehran ilisitisha juhudi za kutengeneza silaha za atomu katika mwaka 2003.

Kwa upande mwingine Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amesema,ripoti hiyo ni tangazo la ushindi kwa mradi wa nyuklia wa Iran.Lakini Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert akishukia ripoti hiyo amekariri kuwa Israel itaendelea kujitahidi kuizuia Iran kujipatia silaha za nyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com