AC Milan klabu bingwa ya dunia | Michezo | DW | 17.12.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

AC Milan klabu bingwa ya dunia

Baada ya Mbrazil Kaka kuitawaza AC Milan jana mabingwa wa dunia ,leo atazamiwa kutawazwa mwanasoka wa dunia.

default

Bayern's Franck Ribery,

Robo-finali ya kombe la CECAFA-kombe la Afrika ya mashariki na kati-challenge cup imeanza leo mjini Dar-es-salaam huku zanuibar Heroes ikiwa imetoa salamu zake kutokaArusha kwa Ruanda.

AC Milan ndio klabu bingwa ya dunia baada ya kuikomea Boca Juniors ya Argentina jana 4-2 mjini Yokohama na stadi wao Kaka atazamiwa kutawazwa leo „mwanasoka bora wa mwaka wa wa dunia“.

Na kocha mjerumni wa Ivory Coast Uli Stielike atumai stadi wa Chelsea , Didier Drogba atakuwa fit kuichezea Ivory Coast katika kombe lijalo la Afrika la mataifa nchinio Ghana, mwezi ujao.

Ni Ramadhan Ali nikiwakaribisha tena katika ulimwengu wa michezo mwishoni mwa wiki.

Tuanze na robo-finali ya challenge Cup-kombe la Afrika mashariki na kati lililohamia Dar-es-salaam kwa robo-finali zilizoanza alaasiri ya leo.

Mwanamichezo wetu George njogopa anatufungulia sasa pazia la robo-finali na msangao uliozushwa hadi sasa na chipukizi-Zanzibar Heroes waliotamba huko Arusha.Je, watatamba pia mzizima ?

Kesho zanzibar ina miadi na Ruanda mjini Dar-es-salaam wakati Uganda ina changamoto na harambee Stars-kenya.

Kenya imeitoa Somali mwishoni mwa wiki kwa mabao 2 na kunusurika kuaga mashindano.

Kocha wa wa Corte d’ Iviore-timu ya Taifa ya Ivory Coast, mjerumani Ulrich Stielike, atakewaongoza tembo hao katika kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana linaloanza januari 20,mwezi ujao, yungali ana matumaini kwamba stadi wa Chelsea ya Uingereza , Didier Drogba atakuwa amepona vya kutosha kuweza kucheza katika kombe la Afrika.Stielike anatumai Drogba atajiunga na kikosi chake nchini Spian mwanzoni mwa mwaka mpya.Mwishoni mwa wiki iliopita, Drogba alifanyiwa opreshini gotini ili kuponesha maumivu ya muda mrefu.Tembo wa Ivory Coast wameangukia kundi moja la B na Nigeria,Mali na Benin.

Nje ya Afrika, AC Milan ya Itali,ni mabingwa wa dunia wa kombe la klabu bingwa .kaka wa Brazil anaetazamiwa jioni ya leo kuvalishwa taji la „mwanasoka bora wa mwaka wa dunia“ kuongezea na taji lake alilovikwa karibuni la ‚golden ball’ la mpira wa dhahabu akiwa mwanasoka bora wa Ulaya, ndie aliekuwa ufungo jana wa ushindi wa mabao 4-2 wa Ac Milan dhidi ya mabingwa wa Amerika kusini-boca Juniors ya Argentina mjini yokohama,japan.

Katika kinyan’ganyiro hicho cha taji la mwanasoka bora wa dunia jioni hii, Kaka mwenye umri wa miaka 25 anakumbana na changamoto kutoka stadi wa Manchester united Christiano Ronaldo wa Ureno pamoja na mshambulizi wa Argentina Lionel Messi.

Hapo kabla, kaka alivikwa taji la mpira wa dhahabu ambalo hasa ni kwa mchezaji wa asili ya ulaya .

Katika Ligi mashuhuri za Ulaya, Bayern munich-wamekwenda likizo ya mwaka mpya na ya x-masi wakiwa mabingwa wa nusu-msimu ingawa wako pointi sawa na Werder Bremen.Licha ya kutoka sare 0:0 jumamosi na Hertha Berlin, Munich itaanza duru ya pili ya msimu ikiwa kileleni mwa Bundesliga.

Bremen iliikomea Leverkusen mabao 5-2 kuwa na pointi 36 sawa na Bayern Munich,ni magoli tu yanayozitenganisha timu hizo mbili.

Munich iliteremka uwanjani jumamosi bila ya nahodha na kipa wao maarufu Oliver Kahn.

Kahn alifungiwa mechi moja na kupigwa faini ya dala 37.500 kwa kuwakosoa wenzake 2 hadharani na kuondoka katika shehe ya x-masi kabla ya wakati ilihali yeye ni nahodha:

Akielezea kwanini amempitishia nahodha wake adhabu hiyo, kocha wa Bayern munich Ottmar hitzfeld alisema:

„Haiwezekani klwa nahodha kuiacha meli yake kabla ya wakati na kwenda nyumbani au kwa safari nyengine.“

Alinun’gunika Ottmar Hitzfeld.

Hamburg inafuata nafasi ya tatu nyuma ya munich na Bremen lakini sasa iko pointi 4 kutoka zilipo Munich na Bremen.Kwani, hamburg ilimudu suluhu tu ya bao 1:1 na chipukizi Cottbus.

Akielezea pigo hilo, kocha wa Hamburg,Huub stevens, alisema:

„Tumetoa sadaka pointi 2 nyumbani kwa Cottbus na inatulazimu kuzirejesha pointi hizo kutoka mchezo mwengine.hii lakini, haitakua rahisihivyo.“ Alisema huub stevens-mholanzi kocha wa hamburg.

Katika premier League-ligi ya Uingereza,manchester united na Arsenal london,zinaongoza sasa Ligi ya Uingereza baada ya jana moja kuizaba Chelsea na mwengine Liverpool kwa bao 1:0.

Mabingwa Manchester waliipiku Liverpool na kuparamia kwa muda mfupi kilelelni mwa Ligi, lakini Arsenal ikasawazisha kwa ushindi mbele ya Chelsea.

Taarifa kutoka Zurich-makao makuu ya FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni zasema Argentina itamaliza mwaka huu ikiwa ndio timu bora kabisa ya dunia-hii ni kwa muujibu wa orodha ya timu bora kabisa za mwezi huu za FIFA.Argentina imepoteza mechi 3 tu kati ya 16 iliocheza mwaka huu .Pigo kali ilipata kutoka mahasimu na majirani zao Brazil katika finali ya Copa America.Brazil licha ya kutawazwa mabingwa wa kombe hilo wameibuka wapili huku mabingwa wa dunia Itali wakiwa nafasi ya tatu.

 • Tarehe 17.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcqE
 • Tarehe 17.12.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CcqE