1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

80% ya wabunge Uganda wapinga

21 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC8K

YAOUNDE:

Rais Paul Biya wa Kamerun ametangaza kuwa Julai 22 itafanyika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge na wa mabaraza ya miji nchini Kamerun.

Kanuni ya rais huyo haikutaja tarehe ya duru ya pili ya uchaguzi.

Katika uchaguzi wa 2002,chama-tawala cha rais Biya (RDPC) kilinyakua ushindi mkuu wa viti 149 kati ya 180 katika Bunge la Taifa.Chama kikuu cha Upinzani Social Democratic party (SDF) kinachoongozwa na John Frau Ndi,kilijipatia viti 22.

Rais Biya alie madarakani tangu 1982,alichaguliwa mara ya mwisho Oktoba 2004 alipojipatia 71% ya kura kwa kipindi cha miaka 7.

KAMPALA:

Taarifa kutoka Kampala,Uganda zasema kuwa, 80% ya wabunge na wengi wao kutoka chama-tawala cha rais Yoweri Museveni,wanapinga mpango wa kuugeuza msitu wa Mabira kuwa shamba la miwa kutengeza sukari.

Uchunguzi uliofanywa kwa wabunge 200 kati ya wote 332 umeonesha 80% wanaupinga mpango huo unaozusha mabishano kufyeka hekta 7,100 za msitu wa Mabira-mbuga ya hifadhi tangu 1932 kugeuka shamba la kutengezea sukari la mwanabiashara wa kihindi Mehta.Wabunge 4 hadi sasa wametiwa nguvuni kwa maandamano ya kupinga mradi huo.