Ziara ya baba mtakatifu Mashariki ya kati | Magazetini | DW | 14.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Ziara ya baba mtakatifu Mashariki ya kati

Kwanini Demjanjuk ahukumiwe ?

default

Pope Benedict XVI na Rais Perez

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo hii yamegusia mada mbali mbali kuanzia ziara ya Baba mtakatifu Benedikt XVI huko Mashariki ya Kati,kuletwa Ujerumani jana kwa John Demjanjuk,anaetuhumiwa uhalifu enzi zanutawala wa Manazi,mkakati wa ulinzi wa Urusi na juhudi za kudhibiti silaha miongoni mwa raia nchini Ujerumani.

Gazetii la FLENSBURGER TAGEBLATT laandika juu ya ziara ya Baba mtakatifu :

"Yule anaeuangalia mwito uliodhahiri wa Baba mtakatifu Benedikt XVI. wa kudai kukomeshwa kuteseka zaidi kwa wapalestina,huyo atatambua huyu ni Kiongozi mkuu wa dini asietenda inavyotarajiwa rasmi na inavyobidi kutenda kisiasa kama ni kipimo cha ujumbe aliouchukua.Ziara yake ngumu ya Mashariki ya kati ,itaacha nyayo zake kwa kuwa tu,Baba mtakatifu hakujiachia kushawishiwa kisiasa. Dhana zisizo sahihi juu ya Baba mtakatifu zinatokana na maoni potofu vichwani mwa baadhi ya watu juu wajerumani.Baba mtakatifu anaacha nyayo zake katika nchi hii takatifu kwa jinsi alivyohiji na jinsi bila kigeugeu alivyotaja dhulma inayopita tena kwa jina ."

Likichambua kusafirishwa jana Ujerumani kutoka Marekani mtuhumiwa wa uhalifu enzi za utawala wa Manazi, John Demjanjuk,gazeti la Emder Zeitung laandika:

"Demjanjuk atafikishwa Mahkamani ikiwa hakutazuka kitu cha kuzuwia hatua hiyo-jambo ambalo kwa mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 89, yawezekana likatokea.Mahkama kwahivyo, iutumie wakati huu kubainisha uhalifu anaotuhumiwa mzaliwa huyo wa Ukraine .Muda haukupita ili kuchunguza kuhilikishwa umma wa watu 29,000.Kwahivyo, kinachoamuliwa hapo si hatima ya Demjanjuk,bali zaidi kuanika hadharani uhalifu uliopita kwa jina la wajerumani ambao bado haukushughulikiwa kikamilifu..."

Gazeti la Volksstimme kutoka (Magdeburg) linatugeuzia mada likichambua kanuni ya muongozo wsa kijeshi enzi ya utawala wa Putin alipokuwa rais namna hii:

"Tumezingirwa na maadui na usoni kabisa ikiwa Marekani na tunaweza tu kukabiliana nao kwa kuunda silaha zaidi.Tangu pale upepo mpya kuanza kuvuma kutoka Washington , hata Moscow imeanza kuregeza kamba.

Mkakati mpya wa kijeshi unatoa sasa mwanya wa kupunguzwa silaha.Hatahivyo, Marekani na Urusi hazitakuwa marafiki wakubwa.Kuwa na ushirika ulio sawa kati yao ni mafanikio makubwa kutarajia..."

Likitumalizia gazeti la Stuttgarter Nachrichten linaijadili sheria ya kudhibiti silaha nchini:Laandika :

"Serikali ya Ujerumani haipigi marufuku watu binafsi kumiliki silaha kutokana na sababu moja tu:Nayo kuwa na ghala moja kubwa ya kurundika bunduki kungegharimu fedha nyingi. Kwa njia hiyo, inasalim amri na kulikwepa tatizo liliopo.Kwani, kwa sababu gani mtu awe na silaha inayoua nyumbani mwake ?"

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com