1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa EU wakutana Copenhagen kuijadili Ukraine

2 Oktoba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi takriban 50 wa Ulaya mjini Copenhagen, kujadili namna ya kuiimarisha Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi

https://p.dw.com/p/51P9F
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Zelensky kukutana na viongozi wa Ulaya kujadili namna ya kuiimarisha nchi yake dhidi ya uvamizi wa UrusiPicha: Julien Mattia/Le Pictorium/MAXPPP/picture alliance

Zelensky anatazamiwa kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa washirika wake wa Ulaya. Watajadili pia vitendo vya uchokozi wa droni za Urusi kuingia kinyume cha sheria nchini Denmark na Estonia.

Zelensky amesema ulaya inakabiliwa na kitisho cha mashambulizi ya droni na ni lazima hatua zichukuliwe

"Nadhani jambo muhimu zaidi kwa sasa ni kwamba Ulaya inakabiliwa na vitisho vya mashambulizi ya droni. Labda sisi ndio tunakabiliwa na mashambulizi makubwa zaidi ya droni duniani. Lakini Ukraine ina uzoefu mkubwa wa kukabiliana na kitisho hicho kwa sababu ya vita. Na bila shaka washirika wetu wakitishiwa sisi hatutakaa kando kuangalia tu."

Awali mawaziri wa fedha wa G7 walifanya mkutano kwa njia ya mtandao na wakaamua kuzidisha shinikizo kwa wanaoendelea kununua kwa kiwango kikubwa mafuta ya Urusi wakisema hilo litaathiri mapato ya Moscow inayoyatumia kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine.