ZANZIBAR:Meli ya Mizigo yahofiwa imezama na wote 14 kufa maji | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ZANZIBAR:Meli ya Mizigo yahofiwa imezama na wote 14 kufa maji

Meli ya mizigo iliyokuwa imetoweka kwenye bahari ya Hindi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja inasemekana huenda ilizama na watu wote 14 waliokuwemo wamekufa.

Kwa mujibu wa waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania Adam Mwakanjuki Meli hiyo ya MV Reef Azania iliondoka Dubai mwezi Juni tarehe 20 ikiwa na wafanyikazi wake wanane raia wa Tanzania , wahindi wawili pamoja na raia wawili wa Myanmar na wapakistan wawili.

Meli hiyo ilikuwa imepakia makontena ya mizigo iliyotarajiwa kusafirishwa katika visiwa vya Usheliusheli kabla ya kugeuza na kutia nanga visiwani Zanzibar mnamo July 8.

Meli hiyo haijafanya mawasiliano yoyote tangu juni 24.Tayari kampuni ya bima imeanza mpango wa kuwalipa familia za waliokuwemo kwenye meli hiyo .Hii ni Meli ya tatu kutoweka katika bahari hiyo ya Hindi tangu mwezi Juni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com