Zaidi ya watu 22 wauwawa | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 25.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Zaidi ya watu 22 wauwawa

---

BAGHDAD

Zaidi ya watu 22 wameuwawa na wengine 30 wamejeruhiwa hii leo baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujiripua ndani ya gari nje ya jengo lenye makaazi ya watu kaskazini mwa Iraq.

Mshambuliaji huyo alivurumisha gari lake ndani ya geti la kuingia kwenye jengo hilo linalomilikiwa na kampuni ya mafuta ya serikali huko kaskazini kwenye mji wa Beiji kiasi kilomita 250 kutoka kaskazini ya mji wa Baghdad.Polisi walijaribu kuzuia gari hilo lisiingie ndani ya eneo hilo lakini hawakufanikiwa.Wengi wa waliokuwa walikuwa ni raia na kiasi cha watoto watatu.Kufuatia shambulio hilo Serikali ya Iraq imetangaza sheria ya watu kutotembea ovyo kwenye mji huo hadi muda usiojulikana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com