Waziri Frank-Walter Steinmeier azungumzia uchaguzi wa Ukraine katika mahojiano na DW | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Waziri Frank-Walter Steinmeier azungumzia uchaguzi wa Ukraine katika mahojiano na DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Steinmeier amesema anatumai kwamba Rais atakaechaguliwa nchini Ukraine atatambuliwa pia na watu wa mashariki mwa nchi hiyo na hivyo kuwezesha kuanzishwa kwa mchakato wa mdahalo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier

Waziri Steinmeier amesema anatumai kwamba uchaguzi utakaofanyika nchini Ukraine Jumapili ijayo utaleta mabadiliko. Amesema ni kwa ajili hiyo kwamba Ujerumani ilifanya juhudi kwa kushirikiana na wote. Ameeleza kuwa siyo Ujerumani pekee iliyofanya juhudi hizo bali wengi wengine pia. Juu ya uchaguzi huo wa Rais nchini Ukraine Waziri Steinmeier ameeleza:

Steinmeier: "Natumai kwamba watu wote wa Ukraine pia wale wa mashariki watakuwa na uwezekano wa kwenda kupiga kura. Pia natumai kwamba meza ya mdahalo itaanzishwa katika jimbo la Donetsk mnamo wiki hii ili kuwafanya watu waelewe kwamba ni kwa njia ya uchaguzi tu kwamba uhalali mpya utaletwa. Na hatimaye Rais atachaguliwa ambae pia atatambuliwa pia mashariki mwa Ukraine."

Ukraine Schachtar Donezk Protest

Maandamano wa wakazi wa mji wa Donetsk

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema uchaguzi wa jumapili nchini Ukraine utaleta mabadiliko na amewataka wapinzani wa serikali ya sasa waonyeshe kwamba uchaguzi huo ni muhimu kwao pia.Lakini amekiri kwamba hali iliyopo ni ngumu.

Steinmeier: "Napenda kusema kwamba kwa vyovyote vile kwamba huo ni mwanzo tu.Kwa sasa tunakabiliwa na hali ambapo pana serikali mpya na uongozi mpya nchini Ukraine uliochaguliwa na Bunge, lakini uhalali wake unapingwa na watu wa mashariki mwa Ukraine.Lakini wakati wote tunawaambia watu hao: ikiwa mnakosoa, basi mnapaswa kuonyesha ari kubwa ya kutambua kwamba kuchaguliwa kwa Rais, kutakuwa na maana ya kuuanzisha mchakato mpya wa uhalali, ambao kwa hatua kubwa utawezesha kuletwa mageuzi ya katiba na kufanyika uchaguzi wa bunge."

Waziri Steinmeier amesisitiza,umuhimu wa uchaguzi badala ya kufikiria vikwazo.

Steinmeier: "Mimi naelekeza makini katika uchaguzi,nataka uchaguzi wa Jumapili ufanyike, na watu wengi washiriki kwa kadri itakavyowezekana "

Juu ya uwezekano wa vikwazo zaidi Waziri Steinmeier ameeleza.

Steinmeier: "Tutaona jinsi hali inavyoendelea kila siku. Lakini kwa sasa silifikirii suala hilo wakati wote.Mimi naweka mkazo juu ya uchaguzi.Nataka uchaguzi huo ufanyike Jumapili ijayo.Nataka watu wengi washiriki kwa kadri itakavyowezekana."

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier pia ameyafafanua malengo ya sera za nje za Ujerumani. Amesema Ujerumani inaibeba sehemu ya wajibu ambayo inaweza kuitekeleza. Ameeleza kwamba matarajio juu ya Ujerumani yanazidi kuwa makubwa kila mwaka hasa kutokana na nguvu zake za kiuchumi. Waziri Steinmeier amesema Ujerumani inajaribu kuitatua migogoro kwa kutumia tathmini za wazi,ili kutafuta masuluhisho badala ya kuyachambulia ndani ya mtoto wameza na kukwama.

Mwandishi: Dagmar Engel

Tafsiri:Mtullya Abdu.

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com