Waturuki waunga mkono mageuzi ya katiba | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.09.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Waturuki waunga mkono mageuzi ya katiba

Kura ya maoni iliyopigwa siku ya Jumapili nchini Uturuki, imeunga mkono mpango wa kufanywa mageuzi katika katiba ya nchi.

Turkish Prime Minister Recep Tayyip Erdogan casts his vote for a referendum on changes to the constitution that was crafted in the wake of Turkey's 1980 military coup, in Istanbul, Turkey, Sunday, Sept. 12, 2010. Turks voted Sunday on whether to amend a military-era constitution in what the government says is a key step toward EU-style democracy, despite opposition claims that the proposed reforms would shackle the independence of the courts. The referendum on 26 amendments to a constitution that was crafted after a 1980 military coup has become a battleground between the Islamic-oriented government and traditional power elites that believe Turkey's secular principles are under threat. The outcome will set the stage for elections next year in a strategically located NATO ally whose regional clout has surged in recent years.(AP Photo/Ibrahim Usta)

Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akipiga kura yake siku ya Jumapili 12 Septemba, 2010.

Kuambatana na Waziri Mkuu Reccep Tayyip Erdogan, matokeo ya mwanzo ya kura hiyo ya maoni, yanaonyesha kuwa mpango huo umeungwa mkono kwa asilimia 58 baada ya asilimia 77 ya Waturuki kujitokeza kupiga kura zao.

Miongoni mwa mageuzi yatakayofanywa, haki za wananchi na udhibiti wa kiraia jeshini utaimarishwa.Kwa mujibu wa Erdogan, mabadiliko hayo ni hatua muhimu kwa Uturuki inayotaka kuingia katika Umoja wa Ulaya. Lakini viongozi wa upinzani wanamtuhumu Erdogan kuwa chama chake cha AKP kinataka kuwa na ushawishi zaidi katika mfumo wa sheria.

Wakati huo huo, mjini Berlin,waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema matokeo ya kura hiyo ya maoni ni hatua muhimu kwa Uturuki kuelekea Ulaya. Hata hivyo,mchakato wa mageuzi unapaswa kushughulikiwa zaidi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com