Watu 92 wameuawa katika mashambulio ya kigaidi | Matukio ya Kisiasa | DW | 23.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Watu 92 wameuawa katika mashambulio ya kigaidi

Polisi nchini Norway, imearifu kwamba watu wasiopungua 92 wameuawa kutokana na mashambulio mawili ya kigaidi.

CORRECTS YEAR Wounded people are treated in the street in the centre of Oslo, Friday July 22, 2011, following an explosion that tore open several buildings including the prime minister's office, shattering windows and covering the street with documents and debris. (Foto:Scanpix, Berit Roald/AP/dapd) NORWAY OUT

Majeruhi wakitibiwa barabarani katika mji mkuu wa Norway, Oslo

Kati ya hao, 84 waliuawa kwenye kambi ya vijana ya chama cha Social Demokratik iiyopo katika kisiwa cha Utoya karibu na mji Mkuu wa Norway, Oslo. Watu hao walipigwa risasi na mtu aliejifanya kuwa polisi.

Mshambuliaji huyo aliingia katika kisiwa hicho jioni ya jana na alianza kufyatua risasi. Polisi walimkamata mtu huyo mwenye umri wa miaka 32, baada ya muda wa nusu saa. Polisi inatuhumu kuwa mtu huyo ndie pia alielifanya shambulio la bomu mjini Oslo. Polisi sasa, inamsaka mtu wa pili anaetuhumiwa kuhusika na mashambulio hayo.

In this photo taken by Vergard M. Aas, a Norwegian crime reporter who responded to the scene of a mass shooting on Utoya Island, Norway, victims lie near the shoreline approximately one hour after police say a man dressed as a police officer gunned down youths as they ran and even swam for their lives at a camp which was organized by the youth wing of the ruling Labor Party, Friday July 22, 2011. Police say the suspect in this shooting set off a fatal explosion hours earlier in the Norwegian capital of Oslo, (Foto:Presse 3.0, Vegard M. Aas/AP/dapd)

Majeruhi waliofyatuliwa risasi katika kisiwa cha Utoya nchini Norway

Muda wa saa 2 kabla ya mauaji kufanyika kwenye kisiwa cha Utoya, watu 7 waliuawa mjini Oslo, baada ya bomu kulipuka kwenye kitongoji cha serikali .Bomu hilo lililipuka karibu na ofisi ya Waziri Mkuu Jens Stoltenberg.

Wakati huo huo mtu aliekuwa na kisu akiwa karibu na waziri Mkuu huyo amekamatwa na polisi.Hapa nchini Ujerumani, Waziri wa mambo ya nje Guido Westerwelle pia ameyalaani vikali mashambulio hayo ya kigaidi.

 • Tarehe 23.07.2011
 • Mwandishi Mtullya, Abdu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RblF
 • Tarehe 23.07.2011
 • Mwandishi Mtullya, Abdu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RblF
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com