WASHINGTON:Wolrlfowitz na hawarawake kufika mbele ya jopo jumatatu
28 Aprili 2007Matangazo
Rais wa benki ya Dunia Paul Worlfowitz na hawara wake watafika mbele ya jopo maalum siku ya jumatatu kujadili kashfa ya kumpandisha cheo na kuongezwa mshahara kidosho huyo kashfa ambayo imezusha miito ya kumtaka Worlfowitz ajiuzulu.
Hapo jana baadhi ya wafanyikazi wa benki kuu ya dunia walizungumzia waziwazi juu ya wasiwasi wao kwamba kashfa hiyo imeshusha hadhi ya uaminifu wao na kazi yao katika kuumaliza umaskini.