WASHINGTON:Iran yailaumu Mareknai kwa kukiuka masharti ya kimatadifa | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Iran yailaumu Mareknai kwa kukiuka masharti ya kimatadifa

Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya benki tatu zinazomilikiwa na serikali ya Iran.

Vikwazo hivyo pia vinazihusisha kampuni zinazomilikiwa na jeshi la Iran pamoja na makamanda sita wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya Iran.

Sababu zilizotolewa na Marekani ni kwamba Tehran inataka kutengeneza silaha za nyuklia na wakati huo huo inaunga mkono ugaidi.

Iran imeilaumu Marekani kwa kukiuka masharti ya kimataifa.

Wizara ya mambo ya nje mjini Tehran imesema kuwa vikwazo hivyo havitafaulu kulidhoofisha taifa hilo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier aliwatolea mwito wapatanishi wa maswala ya nyuklia wa Iran alipokutana nao mjini Hamburg.

Waziri Steinmier amemtaka mpatanishi mpya wa Iran bwana Said Jalili na mtangulizi wake Ali Larijani kuanzisha majadiliano ya ushirikiano na mkuu wa shirika lilano simamia nishati ya nyuklia la umoja wa mataifa Mohamed El Baradei na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com