WASHINGTON:Barua ya alkaida yadakizwa na Marekani ?
8 Oktoba 2005Marekani inasema imedakiza barua ya naibu kiongozi wa mtandao wa alkaida Aiman al Zawahiri.
Katika barua hiyo aliyomtumia Abu Mussab al Zarqawi ,mwakilishi wa alkaida nchini Irak, bwana Zawahiri amesema mikakati inayotumiwa na wapinzani nchini Irak inaweza kusababisha idadi kubwa ya waislamu kuupa kisogo mtandao wa alkaida.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani ameeleza kwamba barua hiyo ni ya kweli bila ya kutoa maelezo zaidi kuhusu kudakizwa kwa barua hiyo.
Katika barua hiyo bwana Zawahiri pia amesema kwamba mtandao wa alkaida unakabiliwa na migogoro katika sekta kadhaa ikiwa pamoja na ya fedha.
Naibu huyo wa Osama Bin Laden katika barua hiyo hasa ameonya dhidi ya mikakati ya kuwateka watu nyara na kushambulia misikiti.