Washington. Marekani kuuza silaha kwa mataifa ya mashariki ya kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington. Marekani kuuza silaha kwa mataifa ya mashariki ya kati.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleeza Rice ametangaza mapendekezo ya mpango mpya wa mauzo ya silaha za Marekani kwa baadhi ya mataifa ya Kiarabu.

Akizungumza kabla ya ziara yake ya siku nne katika eneo la mashariki ya kati akiwa na waziri wa ulinzi Robert Gates , Rice amesema mapendekezo hayo ambayo yatatekelezwa katika muda wa miaka 10 , yatasaidia kuimarisha majeshi ya mataifa yenye msimamo wa kati na kupambana na ushawishi wa al-Qaeda, Hizbollah, Syria na Iran.

Mapendekezo hayo ya mauzo kwa mataifa ya Kiarabu, hususan Saudi Arabia , yatawekwa katika uwiano na ongezeko la asilimia 25 la msaada wa kijeshi kwa Israel, ikiwa pia utatolewa kwa muda wa miaka 10.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com