WASHINGTON: Marekani kuifutia deni Liberia | Habari za Ulimwengu | DW | 14.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Marekani kuifutia deni Liberia

Marekani imesema ina mpango wa kufuta deni la zaidi ya dola milioni 390 inayoidai Liberia.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, ametoa tangazo hilo kwenye mkutano wa wahisani kuhusu Liberia mjini Washington na kuzitaka nchi za magharibi kuzisaidia nchi za Afrika magharibi. Waziri Rice pia amesema rais George W Bush amelitaka bunge la Congress liidhinishe dola milioni 200 kama msaada zaidi kwa Liberia kwa mwaka huu na mwaka ujao.

Vita vya miaka minne nchimi Liberia vilisababisha vifo vya watu takriban laki mbili na kuiharibu miundo mbinu ya nchi hiyo. Liberia ina deni la dola bilioni 3.7

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com