WASHINGTON. Bush ajibu maswali ya waandishi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON. Bush ajibu maswali ya waandishi

Rais George W Bush wa Marekani amezungumzia maswala mbalimbali kuhusu sera za nje za Marekani wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika ikulu ya White House.

Bush alithibitisha kauli ya maafisa wa Marekani kutoka nchini Irak iliyoashiria kwamba Iran inawapa wapiganaji vifaa vya kulipuka vinavyotumiwa kuwauwa wanajeshi wa Marekani nchini Irak.

Rais Bush lakini amekiri kuwa bado haijathibitika kwamba utawala wa Iran ndio unahusika moja kwa moja na utoaji wa silaha hizo.

Kuhusu makubaliano ya pande sita juu ya mzozo wa nyuklia wa Korea Kaskazini Bush amewapuuza wakosoaji wa makubaliano hayo na kusema kuwa mafanikio katika hatua hiyo ya kwanza ni mazuri.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com