Washindwa kukubaliana juu ya Kosovo | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washindwa kukubaliana juu ya Kosovo

Viongozi wa Serbia na wale wa asili ya Waalbania wa Kosovo wameshindwa kufikia makubaliano juu ya jimbo lililojitenga la Serbia .

Katika mazungumzo yaliofanyika hapo jana mjini Brussels Ubelgiji wasuluhishi wa Kosovo wamekataa pendekezo la Serbia la kuwa na mamlaka makubwa ya kujiamulia mambo yake yenyewe na badala yake wamesisitiza kupatiwa uhuru chini ya usimamizi wa Umoja wa Ulaya. Hata hivyo pande zote zimekubali kuendelea na mazungumzo zaidi nchini Austria wiki ijayo.

Kiongozi wa waasi wa zamani wa Waalbania wa Kosovo Hashim Thaci ambaye chama chake kimeshinda uchaguzi wa bunge wa Kosovo hapo Jumapili ametishia kujitangazia uhuru iwapo makubaliano juu ya mustakbali yatashindwa kufikiwa hapo tarehe 10 mwezi wa Desemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com