Wapalestina 6 wauawa katika mashambulizi mapya ya Isreal | Habari za Ulimwengu | DW | 17.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wapalestina 6 wauawa katika mashambulizi mapya ya Isreal

GAZA:

Vikosi vya Israel vimefanya mashambulizi kadhaa ambapo Wapalestina 6 wameuawa.

Kombora ambalo limefyatuliwa na ndege dhidi ya wapiganaji wa Islamic Jihad, inasemekana limeipga gari jingine kwa makosa, na kuwaua; mtoto wa umri wa miaka 13, babake na mjomba wake.Katika eneo la West Bank,vikosi vya Israelvimempiga risasi na kumuua kamanda wa Islamic Jihad-Walid Obeid.Baadae shambulio la ndege katika eneo la Gaza liliwauwa watu wawili ambao ni wanachama wa kundi moja la mgambo.Israel imeapa kuendesha kapeini dhidi ya mashambulizi ya mabomu na maroketi ambayo hutokea Ukanda wa Gaza na West Bank kwa lengo la kuyakomesha.Polisi ya Isreal imesema kuwa maroketi na mizinga inayofikia 47 ilivurumishwa kwa ardhi ya Israel kutokea maeneo ya Gaza na West Bank hiyo jana.Hata hivyo,polisi imesema, makombora ya wapalestina haikusababisha madhara yoyote.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com