Wafungwa zaidi ya 400 waachwa huru | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 25.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Wafungwa zaidi ya 400 waachwa huru

---

BLANTYRE

Zaidi ya wafungwa 400 wameachwa huru nchini Malawi kufuatia msamaha war ais Bingu wa Mutharika kama zawadi ya Xmas kwa familia za watu hao.

Wafungwa hao ambao 15 kati yao walikuwa katika hali mahututi na hawawezi tena kubakia jela walikuwa tayari wametumikia nusu ya kifungo cha jela walichokuwa wamepewa na waliokuwa na tabia nzuri na walikuwa wametenda makosa madogo madogo.Kuachwa huru kwa wafungwa hao zaidi ya 400 kutasaidia kupunguza msongamano wa wafungwa kwenye jela 23 za nchini Malawi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com