1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Brazil zadhamiria kuimarisha ushirikiano

19 Aprili 2026

Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz atakutana na Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva mjini Hanover, ambako wawili hao watafungua rasmi maonesho makubwa ya kimataifa ya biashara Hannover Messe Jumapili jioni.

https://p.dw.com/p/5CRvm
Rais wa Brazil  Lula da Silva  na Kansela wa Ujerumani wanakutana mjini  Hannover 19.14.2026
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Brazil Lula da Silva walipokutana Brazil 07.11.2025Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Baada ya ufunguzi huo viongozi hao wanapanga kufanya mashauriano ya kiserikali Jumatatu wakilenga kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara, ulinzi, teknolojia ya kidijitali, utafiti na ulinzi wa mazingira. Mikataba kadhaa inatarajiwa kutiwa saini katika mazungumzo hayo.

Ushirika wa kibiashara kupewa kipaumbele

Brazil ni moja ya mataifa ambayo serikali ya Ujerumani inataka kuimarisha nayo uhusiano. Taifa hilo ni mshirika wa nne mkubwa wa kibiashara wa Ujerumani na linalenga kujitambulisha katika maonyesho ya Hannover Messe kama taifa kubwa lenye viwanda vilivyosheheni ubunifu, ushindani na linalozingatia maendeleo endelevu.