VIENNA:Hatma ya Kosovo bado haijaamuliwa mazungumzo zaidi mwezi ujao | Habari za Ulimwengu | DW | 23.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VIENNA:Hatma ya Kosovo bado haijaamuliwa mazungumzo zaidi mwezi ujao

Mazungumzo ya hivi karibuni juu ya kuutatua mzozo wa hatma ya jimbo la Kosovo yamemalizika bila ya kupatikana suluhu.

Hata hivyo wapatanishi katika mazungumzo hayo Umoja wa Ulaya,Urussi na Marekani pamoja na wajumbe wa Pristina na Belgrade wamekubaliana kuwa na mazungumzo zaidi mapema mwezi ujao.

Kufuatia mazungumzo ya mjini Vienna Austria wajumbe kutoka jimbo la Kosovo wamewaambia waandishi wa habari kwamba wataendelea kubakia mbali mbali na Serbia.

Wajumbe hao wa Kosovo wametishia kujitangazia uhuru ikiwa pande hizo mbili zitashindwa kufikia muda wa mwisho uliowekwa wa kuwa na makubaliano wa Desemba 10.

Serbia pamoja na mshirika wake Urussi zinapinga jimbo hilo kuwa huru kama ilivyopendekezwa katika mpango wa Umoja wa mataifa.

Aidha Urussi imetishia kutumia kura yake ya Veto katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuzuia hatua yoyote ya utekelezwaji wa mpango huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com