1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Uturuki yatuma wataalam kusaidia kutafuta miili Gaza

17 Oktoba 2025

Uturuki imetuma timu ya wataalam wa kushughulikia majanga kusaidia kutafuta miili iliyo chini ya vifusi huko Gaza. Rais Trump ametoa onyo kwa Hamas juu ya mfululizo wa mauaji ya hivi karibuni katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/52B5e
Ukanda wa Gaza Khan Yunis 2025 | Familia zilizorudi Khan Yunis na kutafuta mali katika eneo lililoharibiwa la Al-Katiba
Mabaki ya vifusi Khan YounisPicha: Abdolrahman Rashad/picture alliance

Uturuki imetuma timu ya wataalam wa kushughulikia majanga kusaidia kutafuta miili iliyo chini ya vifusi huko Gaza,  wakati Rais Donald Trump  wa Marekani akitoa onyo kwa Hamas juu ya mfululizo wa mauaji ya hivi karibuni katika eneo hilo.

Trump ameyataja mauaji hayo kama ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano aliyoyaongoza, ambapo kundi la wanamgambo la Hamas liliwarudisha mateka 20 wa mwisho walionusurika kwa Israel. Hamas imedai kuwa imerejesha miili yote ya mateka lakini miili 19 bado haijulikana iliko na inaaminika kufunikwa chini ya magofu pamoja na idadi kubwa ya Wapalestina.

Hamas imesema kuwa inaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel na wanataka kurejesha miili yote ya mateka iliyosalia Gaza. Wataalam wa Uturuki watasaidia kuitafuta miili ya mateka huku familia zikikasirishwa na Hamas kwa kushindwa kurejesha miili ya jamaa zao.