Utata wa muda wa uokozi nchini Afghanistan | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.08.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Utata wa muda wa uokozi nchini Afghanistan

Utata wa muda wa uokozi nchini Afghanistan

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amesema inaashiria hakuna uwezekano wa kuongezwa kwa muda wa zoezi la kuwaondoa watu nchini Afghanistan baada ya Agosti 31.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amesema inaashiria hakuna uwezekano wa kuongezwa kwa muda wa zoezi la kuwaondoa watu nchini Afghanistan baada ya Agosti 31, wakati ambapo viongozi wa kundi la nchi saba tajiri ulimwenguni - G7 wakijiandaa kwa mkutano wao ombao pia utaujadili mgogoro huo.

Uingereza ndio mwenyeji wa mazungumzo hayo ya dharura, kwa kundi hilo la mataifa tajiri unaofanyika baadae leo hii. Na imesema itaishauri Marekani kurefusha ukomo wa muda wao wa kusalia nchini Afghanistan. Ufaransa nayo imetoa wito wa kufanyiwa marekebisho ratiba hiyo. Lakini saa kadhaa kabla ya mkutano huo wa G7, Wallace amedokeza kwa pamoja Rais wa Marekani, Joe Biden na viongozi wa Taliban, ambao kwa sasa wanashika hatamu ya uongozi mjini Kabul, wameonesha mashaka ya kuendelea kwa shughuli ya uokozi hadi kufikia Septemba.

Uingereza yaokoa zaidi ya 2000 katika kipindi cha masaa 24 nchini Afghanistan.

Zaidi ya hapo Wallace aliseema "Hata hivyo habari njema ni wale tuliowaokoa, ambao ni zaidi ya watu 2,000 katika kipindi cha muda

Indonesien | Flüchtlinge aus Afghanistan protestieren in Jakarta

Waafghanistan wakiandamana dhidi ya Taliban

wa masaa 24 yaliyopita, kiwango hicho ni kikubwa kuliko kile cha watu 700 katika masaa 24 ya kabla ya haya ya sasa. Hii inamaanisha tumewaokoa watu 8,600 tangu kuanza kazi ya uokozi Agosti 14. Na kimsingi tumevuka malengo ya uokozi wa zaidi ya watu 10,000 tangu Aprili, kupitia program ya ARAP.'' Alisema waziri huyo.

Rais Biden amepanga Agosti 31 kuwa ndio tarehe ya mwisho ya kuhitimisha zoezi la uokozi, ingawa aliacha milango wazi ya kurefusha muda huo endapo itahitajika. Hata hivyo, hapo jana Jumatatu kundi la Talban lilionya kwamba halitakubaliana na hatua yoyote ya kurefushwa ya kuongezwa kwa muda huo, ikisema hatua hiyo ni sawa na kuvuka mstari mwekundu. Taliban imekwenda mbali wa kusema kwamba hatua hiyo ni sawa na kurefusha muda wa ukaliwaji wa Afghanistan na wageni.

Umoja wa Mataifa walihusisha kundi la Taliban na ukiukwaji wa haki za binaadam.

Kabla mkutano unaotarajiwa wa G7, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema pamoja na majidiliano yao kujikita katika suala la kichumi kwa mataifa yao, lakini pia jicho litaelekezwa kwa kina Afghanistan.

Katika hatua nyingine mkuu wa masuala ya haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema ana taarifa za uhakika za kufanyika kwa ukiukaji haki za kiutu zinazofanywa na Taliban nchini Afghanistan vikiwemo maujai na vizuizi dhidi ya wanawake.

Wakati hayo yakielezwa Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema umoja huo sasa utaongeza misaada ya kiutu kwa taifa hilo kwa kuchangia nyongeza ya Euro milioni 200 kutoka kiasi cha awali cha Euro milioni 50. Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika tangazo hilo pia atalitoa katika mkutano wa kilele wa mataifa ya G7 baadae leo.

Chanzo: AFP/RTR