1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Utafiti: Wajerumani wana matumaini kuhusu hali zao kiuchumi

26 Mei 2024

Utafiti uliofanywa na muungano wa benki za Ujerumani unaonyesha kuwa Wajerumani wana matumaini chanya kuhusu hali zao za kiuchumi tofauti na hali ilivyokuwa mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4gI9t
Sarafu ya Euro inayotumiwa ndani ya Umoja wa Ulaya
Sarafu ya Euro inayotumiwa ndani ya Umoja wa UlayaPicha: K. Schmitt/Fotostand/IMAGO

Utafiti uliofanywa na muungano wa benki za Ujerumani unaonyesha kuwa Wajerumani wana matumaini chanya kuhusu hali zao za kiuchumi tofauti na hali ilivyokuwa mwaka uliopita.

Muungano huo wa benki za Ujerumani hata hivyo umeeleza kuwa Wajerumani wengi wana mashaka juu ya mustakabali wa kiuchumi wa Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa ujumla kuelekea uchaguzi wa bunge la Ulaya mwezi ujao.

Soma pia: Mataifa ya G7 kutathmini mkopo kwa Ukraine

Asilimia 46 ya Wajerumani 1,000 waliohusishwa kwenye utafiti huo wamesema hali zao za kiuchumi mnamo mwezi Aprili zilikuwa nzuri wakati asilimia 10 wakisema hali ilikuwa sio ya kuridhisha.

Aidha asilimia 37 tu ndio walioridhika na hali zao za kichumi mwaka uliopita.

Utafiti huo umeeleza kuwa, zaidi ya asilimia 54 ya Wajerumani walisema nchi hiyo haijajipanga vizuri kukabiliana na changamoto za kiuchumi siku zijazo huku nusu wengine wakiwa na msimamo kama huo kuhusu Umoja wa Ulaya.