1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yakemea pendekezo la Borrell la kutumia mapato yake

20 Machi 2024

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Maria Zakharova amesema mapendekezo ya Josep Borrell ya kutumia mapato yatokanayo na mali zake zilizozuiwa barani Ulaya ni ujambazi na wizi.

https://p.dw.com/p/4dwhq
Urusi I Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria ZakharovaPicha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Borrell aliyasema hayo jana mjini Brussels na kusisitiza kuwa fedha hizo ambazo zinaweza kufikia euro bilioni 3 kila mwaka, zingelitolewa kupitia Mfuko wa amani wa Ulaya ili kutoa msaada wa kijeshi kwa Kyiv na kuisaidia kuimarisha ulinzi wake.

Hii leo, Ukraine imepokea kifurushi cha kwanza cha msaada wa euro bilioni 4.5 kutoka kwa Umoja wa Ulaya. Hayo yanajiri wakati mapigano makali yameendelea kuripotiwa kati ya Moscow na Kyiv. Urusi imesema ilidungua droni 419 za Ukraine wakati wa uchaguzi huku hali ikizidi kuwa mbala katika eneo la mpakani la Belgorod.