MigogoroMashariki ya Kati
UN yalaani vurugu zinazoshuhudiwa Mashariki ya Kati
28 Februari 2026
Matangazo
Aidha Turk amesema viongozi mbalimbali wamekuwa wakitumia madaraka vibaya na kutoa kipaumbele kwa matumizi ya nguvu kutatua mizozo, hali inayopelekea kuongezeka kwa idadi ya mizozo kote duniani.
Turk amesema idadi ya migogoro inayohusisha silaha imeongezeka maradufu tangu mwaka 2010 na kufikia karibu migogoro 60, huku akitamatisha kuwa kwa sasa dunia inazidi kuwa eneo hatari zaidi.
Aidha, Umoja wa Afrika na mataifa mengine kama Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Brazil na mengineyo yametoa wito wa kusitisha mashambulizi huko Mashariki ya Kati na kurejea kwenye mazungumzo.