1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yaripoti shambulio la droni katika mpaka wa kaskazini

14 Juni 2026

Mamlaka nchini Israel zimesema leo kwamba wanamgambo wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon, wamefanya shambulio jingine la droni huko kaskazini mwa Israel.

https://p.dw.com/p/5FMcv
Lebanon Kfar Tibnit 2026 | Moshi baada ya shambulio la anga la Israel kusini mwa Lebanon
Moshi ukifuka kutoka eneo la shambulio la anga la Israel lililolenga kijiji cha kusini mwa Lebanon cha Kfar Tibnit mnamo Juni 13, 2026.Picha: Abbas Fakih/AFP

Mamlaka nchini Israel zimesema leo kwamba wanamgambo wa kundi la Hezbollah la nchini Lebanon, wamefanya shambulio jingine la droni huko kaskazini mwa Israel. Jeshi la Israel lilisema milipuko miwili imerekodiwa ndani ya eneo la Israel karibu na mpaka na Lebanon, lakini hakuna majeruhi walioripotiwa.

Ving'ora vya tahadhari vilisikika mapema katika miji kadhaa kando ya mpaka wa kaskazini wa Israel. Shirika la habari la Israel la Ynet limeripoti kuwa ndege isiyo na rubani ilipiga karibu na mji wa mpakani wa Shlomi.

Waziri wa fedha wa Israel mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich, amemtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kutumia mkakati wa mbinu kubwa sana ya kijeshi ya Dahiya dhidi ya maeneo yanayoaminika kuwa na wapiganaji wa Hezbollah katika vitongoji vya kusini mwa Beirut.