Umeme wa kudumu bado donda-ndugu Afrika ya Mashariki | Masuala ya Jamii | DW | 06.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Umeme wa kudumu bado donda-ndugu Afrika ya Mashariki

Licha ya ahadi kadhaa za serikali za Afrika ya Mashariki kulimaliza tatizo la umeme nchini humo, hadi leo nchi za eneo hilo zingali zinaishi kwa upungufu mkubwa wa umeme na, hivyo, kuchangia kuzirudisha nyuma kiuchumi.

Majenereta yanapokuwa kimbilio kwa umeme

Majenereta yanapokuwa kimbilio kwa umeme

Othman Miraji anajadiliana na wataalamu wa masuala ya nishati kutoka Afrika ya Mashariki juu ya kiini cha tatizo la umeme kwenye eneo hilo na njia zinazoweza kulitatua, wakizingatia ukweli kuwa bila ya umeme wa uhakika na wa kudumu, hakuwezi kuwa na maendeleo.

Mtayarishaji: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com