1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yahimiza suluhu ya kidiplomasia mzozo wa Iran

23 Februari 2026

Rais Donald Trump anazidi kutoa vitisho vya kuishambulia kijeshi Iran wakati Umoja wa Ulaya ukihimiza mchakato wa kidiplomasia kupewa nafasi kupata suluhu

https://p.dw.com/p/59G3e
Manuari ya kijeshi ya USS Abraham Lincoln  ikiwa imebeba madege ya kivita
Marekani imepeleka manuari zake za kijeshi katika eneo la ghuba huku maelfu ya wanajeshi wake Mashariki ya kati wakiwekwa tayariPicha: Shepard Fosdyke-Jackson/US Navy/AFP

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas ametowa wito wa kuzingatiwa suluhu ya kidiplomasia kuhusu Iran, kabla ya kuanza tena kwa mazungumzo mengine kati ya Iran na Marekani wiki hii.

Wito huo umetolewa chini ya kiwingu cha vitisho vilivyotolewa na rais Donald Trump dhidi ya Tehran.Iran yasema huenda ikakutana na Marekani jijini Geneva Alhamisi

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu katika Umoja wa Ulaya amesisitiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya hiyo, kwamba Ulaya ina mambo mengi na  haitaki kuona vita vingine.

Jana waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Aragchi alisema kwamba ufafanuzi wa kile kinachoweza kuwa mpango wa makubaliano, unaandaliwa kabla ya mazungumzo yatakayofanyika siku ya Alkhamisi, chini ya usimamizi wa Oman.