Ujumbe wa Pakistan uko Tehran ukitarajia mazungumzo
16 Aprili 2026
Hii ni katika hatua ya hivi karibuni ya kupunguza mivutano huko Mashariki ya Kati na kupanga awamu ya pili ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran baada ya karibu wiki saba za vita.
Pakistan imeibuka kama mpatanishi muhimu baada ya kuwa mwenyeji wa mazungumzo kati ya Marekani na Iran mjini Islamabad.
Mamlaka zinasema mazungumzo hayo yalisaidia kupunguza tofauti zilizoko kati ya mataifa hayo mawili yaliyo kwenye mzozo.
Na sasa wapatanishi wanatafuta kufanyika awamu nyengine ya mazungumzo kabla muda wa mwisho kufika wiki ijayo.
Ikulu ya White House imesema awamu nyengine ya mazungumzo huenda ikafanyika nchini Pakistan ingawa hakuna uamuzi uliofanyika kufikia sasa iwapo kufanyike mazungumzo kwa mara nyengine.
Licha ya vizuizi hivyo vya Marekani katika bandari za Iran, maafisa wa kikanda wanaripoti kuwa hatua zinapigwa huku maafisa ambao hawakutaka kutambulishwa wakisema, Marekani na Iran wana "makubaliano ya msingi" ya kuongeza usitishwaji mapigano ili kutoa fursa zaidi ya diplomasia.