1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapatanishi kurefusha usitishaji mapigano Mashariki ya Kati

Josephat Charo
15 Aprili 2026

Wapatanishi wamekaribia Jumatano kuongeza muda wa kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran na kuanzisha tena mazungumzo ili kuokoa makubaliano dhaifu ya wiki mbili.

https://p.dw.com/p/5CEPr
Juhudi zinaendelea kurefusha muda wa usitishaji mapigano kati ya Marekani na Iran.
Juhudi zinaendelea kurefusha muda wa usitishaji mapigano kati ya Marekani na Iran.Picha: Sha Dati/Xinhua/IMAGO

Wapatanishi wamekaribia Jumatano kuongeza muda wa usitishaji mapigano kati ya Marekani na Iran na kuanzisha tena mazungumzo ili kuokoa makubaliano hayo dhaifu kabla ya kufika mwisho wiki ijayo. Afisa mkuu wa jeshi la Iran alitishia kusimamisha biashara katika eneo hilo ikiwa Marekani haitaondoa mzingiro wa kijeshi wa majini.

Afisa mkuu wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu hakuruhusiwa kujadili hadharani mazungumzo hayo nyeti, amesema Marekani haijakubali rasmi kuongeza muda wa kusitisha mapigano na kwamba mazungumzo na Iran yanaendelea.

Kamanda wa kamandi ya pamoja ya jeshi la Iran, Ali Abdollahi, ameonya kwamba Iran itazuia kabisa mauzo ya nje na bidhaa zinazoingizwa katika eneo la Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Oman na Bahari ya Shamu ikiwa jeshi la Marekani halitaondoa kizuizi chake kwenye bandari za Iran.