1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yawaambia wakulima wanaoandamana 'hakuna fedha'

15 Januari 2024

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner amesema kuwa serikali haina fedha za kuongeza ruzuku kwenye sekta ya kilimo.

https://p.dw.com/p/4bGIE
Waziri wa Kilimo Ujerumani Christian Lindner amewaambia wakulima kwamba hawezi kuwaahidi msaada zaidi wa serikali kutoka kwenye bajeti ya taifa.
Waziri wa Kilimo Ujerumani Christian Lindner amewaambia wakulima kwamba hawezi kuwaahidi msaada zaidi wa serikali kutoka kwenye bajeti ya taifa.Picha: Monika Skolimowska/dpa/picture alliance

Lindner aliyasema hayo leo wakati akiwahutumia maelfu ya wakulima waliokusanyika katika mji mkuu Berlin katika kilele cha maandamano yao ya wiki nzima kupinga mpango wa serikali kuondoa ruzuku ya kodi kwenye dizeli wanayotumia.

Waziri huyo wa fedha amewaambia wakulima waliokuwa wakimzomea, kuwa hawezi kuwaahidi msaada zaidi wa serikali kutoka kwenye bajeti ya taifa.

Shughuli za kawaida mjini Berlin zilivurugwa kutokana na maandamano hayo, ambapo karibu wakulima 10,000 wakiwa na malori na matrekta yao walilijaza eneo la Lango kuu maarufu la Brandenburg.

Waandamanaji hao wanaiongezea shinikizo serikali ya mseto ya Kansela Olaf Scholz wakati ikipambana kuutatua mzozo wa bajeti na kuyadhibiti makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia.