1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yachukua nafasi ya tatu Ulaya na kufuzu Olimpiki

29 Februari 2024

Timu ya taifa ya kandanda Ujerumani kwa wanawake, imejikatia tiketi ya kushiriki mashindano ya mwaka huu ya Olimpiki mjini Paris baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika mashindano ya wanawake ya Nations League.

https://p.dw.com/p/4d0Eb
Kandanda la wanawake Lena Oberdorf Timu ya Taifa
Mchezaji wa Ujerumani Lena OberdofPicha: Hansjürgen Britsch/Baumann/IMAGO

Klara Brühl na Lea Schüller ndio waliowafungia Ujerumani mabao yao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Uholanzi usiku wa kuamkia leo.

Ujerumani sasa imechukua nafasi moja iliyokuwa imesalia kwa Ulaya katika mashindano hayo yatakayofanyika katika msimu wa majira ya joto.

Mabingwa wa dunia Uhispania ndio walioibuka mabingwa wa mashindano hayo ya Nations League baada ya kuwalaza Ufaransa 2-0.

Mchezaji bora duniani kwa wanawake Aitana Bonmati ndiye aliyefunga bao la kwanza kisha la pili la Uhispania likatiwa kimyani na Mariona Caldentey. Uhispania na Ufaransa tayari walikuwa washafuzu Olimpiki.