1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaanzisha sherehe za miaka 30 ya muungano

Sekione Kitojo
5 Septemba 2020

Ujerumani imeanzisha mlolongo wa matukio Jumamosi (05.09.2020) kuadhimisha miaka 30 ya kihistoria kwa taifa hilo tangu pale Ujerumani mbili zilipoungana tena, sherehe ambazo zimefifishwa na janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3i2Q0
Deutschland Eröffnung EinheitsEXPO Potsdam
Picha: imago images/C. Spicker

Bila shaka, badala  ya  kuadhimisha  muungano  hapo Oktoba 3, siku inayofahamika kama  Siku ya Umoja, mlolongo wa  matukio  madogo madogo  yanapangwa  katika  mwezi  mzima, kuepusha mikusanyiko mikubwa  na  kupunguza kitisho cha  kusambaa kwa  COVID-19.

Deutschland Eröffnung EinheitsEXPO Potsdam
Maonesho ya Umoja wa Ujerumani katika mji wa Potsdam , wakiweka maandishi ya "W i r" ikiwa na maana sisi.Picha: imago images/C. Spicker

Potsdam , mji  mkuu  wa  jimbo  la  mashariki  mwa  Ujerumani  la Brandenburg, utakuwa ukiangiliwa kwa karibu  katika  sherehe  hizi za  mwaka  2020.

Matukio ya  mwaka  huu  ya  muungano  pia  yanakuja  chini  ya mwaka  mmoja  baada  ya  Ujerumani  kuadhimisha  miaka  30  ya kuvunjika  kwa  ukuta  wa  Berlin, ikiwa ndio  wakati  muhimu  katika historia  ya  taifa  hilo  ambao ulisafisha  njia  katika  kufikisha mwisho  mgawanyiko uliotokea  nchini  humo  katika  wakati wa  vita baridi.

Lakini badala ya  kuneemeka kwa hali  ya  nchi  kama  ilivyoahidiwa na  kansela  wa  zamani  wa  Ujerumani  Helmut Kohl  kufuatia kuanguka kwa  ukuta, muungano  umethibitisha  kuwa ni mradi ghali na wenye  utata  kwa  taifa  hilo  lenye  uchumi  mkubwa  katika bara la  Ulaya.

Muungano wa Ujerumani 

Bado kuna  uungwaji  mkono  mkubwa  katika  taifa  hilo  kwa  ajili  ya muungano, ambao umeweka  kando  zaidi ya miaka  40 ya ukomunist  katika  eneo  la  mashariki  mwa  nchi hiyo na  kusaidia Ujerumani  kuchukua jukumu  la  mbele  katika  medani  ya  kimataifa.

BdT Deutschland  Potsdam Weg zur Einheit
Rangi za bendera ya Ujerumani katika maonesho ya Potsdam ya Umoja wa UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa/S. Stache

Hata  hivyo , miaka  30  baada  ya  oande  mbili  za  Ujerumani kuungana  tena, tofauti kubwa  za  kijamii  na  kiuchumi  zinaendelea kuwapo  kati ya  maeneo  ya  nchi  hiyo  ya  mashariki  na magharibi.

Taifa  hilo  pia  linapambana  na mgawanyiko  mkubwa  wa  kisiasa na  kuna  hofu kuwa  sherehe  za  muungano  zinaweza zikachafuliwa na  makabiliano  kati ya  makundi  ya  siasa  kali  za mrengo wa  kulia  pamoja  na  watu  wanaofanya  maandamano  ya kupinga  hatua  zinazochukuliwa  kudhibiti  virusi  vya  corona pamoja na   waandamanaji  wanaopinga makundi  hayo.