1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Qatar zatia saini makubaliano ya gesi

29 Novemba 2022

Qatar na Ujerumani zimetia saini makubaliano ya kusafirishwa gesi asili ya kimiminika kutoka Doha kwenye nchi hiyo yenye nguvu kubwa kiuchumi barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4KDZO
Deutschland | Nord Stream 1 Station Lubmin
Picha: Odd Andersen/AFP/Getty Images

Ujerumani inapambana kutafuta msambazaji mbadala wa gesi baada ya Urusi kukatisha usambazaji wa gesi yake kwa Ujerumani wakati wa vita vya Ukraine vinavyoendelea.

Usambazaji wa gesi hiyo kutoka Qatar utaanza mwaka 2026 ingawa haikutajwa gharama zitakazohusika.

Makubaliano hayo yanazihusisha Kampuni ya nishati inayosimamiwa na serikali ya Qatar pamoja na kampuni ya ConocoPhillips ambayo ina hisa katika vinu vya gesi asilia katika pwani ya ghuba ya uajemi ambayo inapakana na Iran.

Nchi za Ulaya zimekuwa zikiiunga mkono Ukraine baada ya uvamizi wa Urusi mnamo mwezi Februari, na Urusi imekatiza usambazaji wa gesi yake asili ya kimiminika ambayo inatumika katika mifumo ya kuleta joto majumbani, kuzalisha umeme pamoja na kundesha shughuli za kiviwanda.

Ujerumani ni moja ya nchi ambazo haijapokea gesi ya aina yoyote kutoka Urusi tangu mwishoni mwa mwezi Agosti.