Uguriki yaidhinisha muswaada wenye utata kuhusu malipo ya uzeeni | Habari za Ulimwengu | DW | 21.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Uguriki yaidhinisha muswaada wenye utata kuhusu malipo ya uzeeni

-

ATHENS

Bunge nchini Ugiriki limeidhinisha muswaada wa mageuzi wenye utata kuhusu malipo ya uzeeni uliowasilishwa bungeni na upande wa serikali baada ya wiki kadhaa za migomo na maandamano ya vyama vya wafanyikazi nchini humo.Serikali imepuuza ongezeko la wimbi la upinzani wa wananchi ambao ulisabbisha mgomo mkubwa wa kitaifa siku ya jumatano ikisema kwamba hatua hiyo ilihitajika kufikiwa ili kuunga mkono mfumo wa usalama wa huduma za kijamii ambao wataalamu wanasema unaelekea kusambaratika katika kipindi cha miaka 15. Muswaada huo ulipitishswa hapo jana na idadi kubwa ya wabunge lakini vyama vingi vya wapinzani viliupinga muswaada huo ikiwa ni pamoja na chama kikuu cha upinzani cha kisosholisti ambacho hakikupiga kura.Hata hivyo hatua hiyo ya kuidhinishwa muswaada huo huenda ikakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com