Ufaransa na Uengereza zataka kushirikiana katika fani ya kijeshi | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.11.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ufaransa na Uengereza zataka kushirikiana katika fani ya kijeshi

Madola mawili makuu ya kinuklea ya Ulaya ya magharibi-Ufaransa na Uengereza yanapanga kuanzisha ushirikiano wa aina pekee wa kijeshi kati yao licha ya kupunguza bajeti zao za ulinzi

default

Waziri mkuu wa Uengereza David Cameron

Uingereza na Ufaransa leo watatia saini mikataba miwili ambayo kwa mara ya kwanza itatoa nafasi kwa nchi hizo mbili kushirikiana katika masuala ya ulinzi, ikiwemo kuundwa kwa jeshi la pamoja, kugawana manowari za kubebea ndege za kivita pamoja na ushirikiano wa karibu wa utafiti wa nyuklia.

Waziri Mkuu wa Uingereza na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy watatia saini mikataba hiyo miwili mjini London ambayo itayapa nafasi mataifa hayo mawili kuwa na usemi mkubwa katika jukwaa la kimataifa licha ya kupunguza bajeti zake za ulinzi.

Akizungumza bungeni hapo jana Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema ana amini kwamba ushirikiano huo wa nchi yake na Ufaransa utakuwa wa manufaa kwa maslahi ya nchi zote mbili.

Majirani hao wawili pia wametetea makubaliano baina yao wakisisitiza kuwa majeshi yao hayatapoteza lile jukumu la kutetea maslahi ya kila taifa licha ya kuwa kikosi cha pamoja.

Akisisitiza hilo Cameron alisema nikimnukuu '' Ushirikiano ndio tutafanya lakini haimaniishi tutapoteza uhuru wetu kama taifa.'' mwisho wa kumnukuu.

Wakizungumzia ushirikiano katika masuala ya nyuklia- Afisi ya rais wa Ufaransa ilisema hatua zote zitakazochukuliwa zitaheshimu uhuru na mamlaka ya nchi zote mbili. Mkataba wa kwanza utashughulikia masuala ya ulinzi- ikiwa ni kuundwa kwa kikosi kinachopelekwa vitani ugenini, kutumia pamoja manowari zinazobeba ndege za vita, kutengeneza ndege za uchukuzi pamoja na ushirikiano katika daraja ya uwakala.

Mkataba wa pili unazungumzia mpango wa kubadilishana teknologia ya kufanyia majaribio silaha za nyuklia, ingawa maafisa wa nchi zote mbili wamesisitiza hili halimaanishi Uingereza na Ufaransa sasa watabadilishana siri zao za nyuklia au kupeana alama zao za siri za manowari zao za nyuklia.

Mpango huu wa ushirikiano kati

Frankreich Wirtschaft Banken Nicolas Sarkozy

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa

ya mahasimu hao wa jadi umekuwa ukiandaliwa kwa muda mrefu na umeharakishwa zaidi na mahitaji ya nchi zote mbili kubana matumizi yake baada ya msukosuko wa kiuchumi. Uingereza na Ufaransa zimelazimika kupunguza bajeti ya majeshi yake ili kukabiliana na nakisi kubwa katika bajeti zao. Lakini pia wanasisitiza hawataki kudhoofisha ushawishi wao katika jukwaa la kimataifa.

Kikosi hicho cha jeshi la pamoja kitakuwa na wanajeshi kati ya 3,500 hadi 5,000 na kitaanza mafunzo mwaka ujao na kitakuwa kinatumiwa kwa kusudi maalum na kuongozwa na Kamanda mmoja atakayekuwa anazungumza lugha ya kiingereza.

Na kuanzia mwaka wa 2020 Uingereza na Ufaransa watakuwa wanatumia kwa pamoja manowari za kubebea ndege za vita. Kwa kuwa kila nchi ina manowari moja, kila mmoja wao ataweza kutumia manowari ya mwenzake pale yake itakapokuwa inatengenezwa.

Mwandishi: Munira Muhammad/ AFPE

Mpitiaji: Hamidou Oummilkheir

 • Tarehe 02.11.2010
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pw8h
 • Tarehe 02.11.2010
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Pw8h

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com