Uchunguzi waendelea kubaini sababu ya ajali ya ndege London | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Uchunguzi waendelea kubaini sababu ya ajali ya ndege London

Wachunguzi wa usalama wanaendelea kutafuta kilichoisababisha ndege ya abiria kulazimika kutua ghafla katikauwanja wa ndege wa Heathrow mjini London Uingereza hapo jana.

Abiria wote 136 na wafanyakazi 16 wa ndege hiyo aina ya Boeing 777, ya shirika la ndege la Uingereza, British Airways, walinusurika. 18 kati yao walipata majeraha madogo na kutibiwa.

Ndege hiyo ilikuwa imetoka mjini Beijing China ikielekea mjini London. Maafisa wa Scotland Yard, wamesema hakuna ushahidi kwamba tukio hilo lina uhusiano wowote na ugaidi.

Ajali hiyo ilisababisha safari za ndege zaidi ya 200 kucheleweshwa ikiwa ni pamoja na safari ya waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown kwenda China.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com