Tuzo ya fizikia ya Nobel ndiyo mada iliyohanikiza magazetini hii leo. | Magazetini | DW | 10.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Tuzo ya fizikia ya Nobel ndiyo mada iliyohanikiza magazetini hii leo.

Mjerumani Peter Grünberg na uvumbuzi wake uliopelekea kubuniwa computor ndogo ndogo

Tuzo ya fizikia ya Nobel ndiyo mada iliyohanikiza magazetini hii leo.

Tuzo ya mwaka huu ya Nobel kwa fani ya fizikia ametunukiwa mjerumani Peter Grünberg na mfaransa Albert Fert.Kwa mujibu wa taasisi ya kifalme ya Sweeden inayoshughulikia masuala ya sayansi mjini Stockholm,wateule hao wawili wanatunukiwa zawadi ya Nobel kwa kugundua nguvu kubwa ya ukinzani wa smaku.Ugunduzi wao ndio uliopelekea kubuniwa disk ngumu ya computa yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi.

Uamuzi wa kamati kuu ya Nobel umewashughulisha mno wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND limeandika:

“Mafanikio haya ni ya shani sawa na kutawazwa timu ya kambumbu ya wanawake mabingwa wa dunia-na kwa Ujerumani,bila ya shaka ni muhimu.Bila ya kutaka makubwa,Peter Grünberg na wenzake pamoja na wafanyakazi wa kituo cha utafiti cha Jülich,walinyanyua bilauri ya mvinyo kusherehekea tukio hilo,mvinyo uliokua umesalia toka sherehe kama hizo.Ilikua mwaka 2005 tuu pale mtaalam wa fizikia wa kutoka München Theodor Hänsch alipotunukiwa pia zawadi ya Nobel .Na sasa mjerumani mwengine pia anatunukiwa zawadi hiyo ya fahari kupita kiasi katika fani ya kisayansi.Ni sifa na jaza kubwa hii kwa shughuli za utafiti wa kina wa kisayansi kwa Ujerumani.

Gazeti la Die WELT linaandika:

„Hongera Dr. Grünberg“,na angalia yaliyopita:Kila kwa mara tunasikia malalamiko kwamba watafiti wanatunukiwa zawadi ya Nobel kwa kazi walizofanya muongo mzima uliopita.Pengine ni kweli;hata hivyo hali ya kuvuta wakati imezusha matumaini mema.Pindi Bwana Grünberg angetunukiwa zawadi hiyo ya Nobel mwaka ule ule alipofanikiwa katika ugunduzi wake,yaani mwaka 1988,basi bila ya shaka mjadala mkubwa ungefuatia.Usingekua tena mjadala wa kisayansi kuhusu uvumbuzi wa ukinzani mkubwa wa nguvu za smaku unaoifanya Computor izidi kuwa ndogo,ungegeuka mjadala wa kisiasa na jamii.Wakati ule bado kulikua na hofu kubwa na wasi wasi kuelekea mtambo wa Computor ,watu wakiamini zitasababisha nafasi za kazi kuteketezwa.“

„Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linaandika:

„Tuzo ya Nobel kwa Peter Grünberg isiwe sababu kwa waziri wa utafiti na taifa kwa jumla kuvuta wakati.Sio lazma watu wajenge kumbusho kwa heshma yake karibu na lango la Brandenburg mjini Berlin.Pekee kujishughulisha zaidi na shughuli zake ingetosha.Grünberg anafabnya kila juhudi na kudadisi kila kwa kwa mara mjini Jülich kile kinachohitajiwa zaidi na jamii yetu inayozidi kukongaa.Ana umri wa miaka 68 ,hata hivyo kila wakati hatoki kwenye maabara ili kama anavyosema mwenyewe“-kufuatana na wakati na kujifunza kutoka kwa vijana.Ni shujaa wa kweli wa taifa.“

Gazeti la GENERAL ANZEIGER la mjini Bonn linaandika:

„Tuzo ya Nobel kwa Grünberg inatupa moyo tusiwe woga mbele ya elimu ya fizikia na hesabu.Tunahitaji motisha kubwa zaidi ya kisayansi ,tena kuanzia shule za chekechea.Ni jambo la maana kuwekeza katika sekta hiyo.Kwa namna hiyo pengine wanawake pia wa Ujerumani, siku za mbele watakua miongoni mwa washindi wa zawadi ya Nobel .Kwasababu miongoni mwa washindi wa tuzo hiyo,wanawake ni wachache.

 • Tarehe 10.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C7lR
 • Tarehe 10.10.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C7lR