1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump asema mwafaka kuhusu Greenland umefikiwa

22 Januari 2026

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa amefikia makubaliano ya mkakati unaomridhisha kuhusu Greenland.

https://p.dw.com/p/57CoE
U.S. President Trump Attends World Economic Forum In Davos
Picha: Chip Somodevilla/Getty Images

Trump ameyasema hayo wakati ambapo pia amedai kuwa hatotumia nguvu kukichukua kisiwa cha Greenland na pia kudai kuwa hatoziwekea tena ushuru bidhaa za mataifa nane ya Ulaya yaliyokuwa yanaupinga mpango wake wa kuitwaa Greenland.

Akizungumza na kituo cha habari cha Marekani CNBC, Trump amesema makubaliano hayo ni ya muda mrefu na kila mmoja ameyafurahia ila hakutoa taarifa zaidi na hakusema pia iwapo hiyo inamaanisha kuwa Marekani itakuwa na udhibiti wa kisiwa hicho cha eneo la Arctic.

Trump ameyasema yote hayo baada ya mkutano huko Davos na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte ambaye kupitia msemaji wake, ameyathibitisha hayo aliyoyasema Trump.