Timu ya Togo yarejea nyumbani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 11.01.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Timu ya Togo yarejea nyumbani

Timu ya taifa ya kandanda ya Togo imerejea nyumbani, kutoka Angola ilikojitoa katika michuano ya Afrika kufuatia shambulio dhidi yao lililofanywa na waasi katika mji wa Cabinda.

Timu ya taifa ya Togo

Timu ya taifa ya Togo

Timu hiyo imerejea ikiwa na miili ya kocha msaidizi na afisa habari wa michezo ambao pamoja dereva wa basi lao waliuawa katika shambulio hilo hapo siku ya Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Togo Gilbert Fossoun Houngbo alitangaza kujitoa kwa nchi hiyo ingawaje wachezaji walitaka kuendelea na mashindano.

Naye Waziri wa michezo wa Togo Christophe Tchao akizungumz na waandishi wa habari kabla ya kupanda ndege iliyotumwa na serikali yao, alisema kuwa ameliomba shirikisho la soka barani Afrika CAF kuangalia uwezekano wa kuiweka tena nchi hiyo katika ratiba ya michuano hiyo baada ya siku tatu za maombolezi.

Mwandishi:Aboubakary Liongo

Mhariri:Thelma Mwadzaya

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com