Timu ya Schalke yaongoza Ligi ya Kandanda ya Ujerumani. | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Timu ya Schalke yaongoza Ligi ya Kandanda ya Ujerumani.

Michezo:

Katika ligi ya kandanda hapa Ujerumani, timu ya Schalke jana ilijipatia goli katika dakika za mwisho za mchezo na kuibwaga Armenia Bielefeld bao moja kwa bila, hivyo kuwa juu kabisa ikongoza ligi. Katika mechi nyingine, bingwa wa mwaka jana, Bayern Munich, iliikanyaga Mainz kwa mabao manne kwa bila; Berlin iliitwanga Eintracht Frankfurt bao moja kwa bila; Nuremberg iliifunga Hannover mabao matatu kwa moja, na Aachen ilikwenda sare na Hamburg mabao matatu kwa matatu; pia Cottbus ilienda sare na Stuttgart bila kwa bila.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com