TEHRAN:Iran kuhudhuria mkutano juu ya Iraq,Misr | Habari za Ulimwengu | DW | 30.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN:Iran kuhudhuria mkutano juu ya Iraq,Misr

Iran itahudhuria mkutano wa kimataifa juu ya Iraq utakaofanyika katika eneo la kitalii la Sharm el Sheikh nchini Misri siku ya alhamisi.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Mohammed Ali Hosseini amesema kupitia televisheni ya taifa kwamba ujumbe wa Iran utaongozwa na waziri wa mambo ya nje wan chi hiyo Manoucher Mottaki.

Tangazo hilo limetolewa muda mfupi baada ya mjumbe wa Iran Ali Larijani kuwasili mjini Baghdad kwa ajili ya mkutano wa siku tatu kujadili masuala mbali mbali ikiwemo uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolleza Rice ambaye pia atahudhuria mkutano wa Misri hajapinga kukutana na bwana Mottaki.Lakini akizungumza kwenye televisheni ya Marekani bibi Rice alisema mkutano wowote na baina yake na bwana Mottaki utahusu tu masuala ya Iraq na wala hautagusia juu ya uhusiano baina ya Iran na Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com