TEHERAN : Mkutano juu ya Maangamizi Makuu wakosolewa
12 Desemba 2006Matangazo
Ujerumani,Israel na Marekani zimekosoa vikali mkutano unaofanywa katika mji mkuu wa Iran, Teheran juu ya Maangamizi Makuu.Rais wa bunge la Ujerumani Lammert katika hati aliompelekea rais Ahmedinejad amesema,propaganda za kibaguzi kuhusu Uyahudi zimepewa jukwaa rasmi.Israel nayo imesema mkutano huo hauna haya.