Tanzania: Wafuasi wa chama cha upinzani CUF wataka kuandamana jijini Dar es Salaam | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Tanzania: Wafuasi wa chama cha upinzani CUF wataka kuandamana jijini Dar es Salaam

Chama Kikuu cha upinzani Tanzania CUF kimepanga kufanya maandamano kudai kuweko tume huru ya uchaguzi.

default

Profesa Ibrahim Lipumba azungumza na waandishi ya habari mjini Dar es Salaam

Katika mkutano na waandishi wa habari hii leo mjini Dar es Salaam, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani katika Tanzania, CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alitangaza kwamba kesho wafuasi wa chama chake watafanya maandamano yatakayopitia katika barabara za Dar es salaam hadi ofisi ya msajili wa vyama vya kisiasa kudai kuweko tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania.
Othman Miraji alizungumza na Profesa Lipumba kutaka ufafanuzi zaidi juu ya madhumuni ya maandamano hayo.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com