Taasisi ya Goethe nchini Kenya yafungua milango yake kwa umma | Masuala ya Jamii | DW | 18.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Taasisi ya Goethe nchini Kenya yafungua milango yake kwa umma

Shirika la Ujerumani linalohusika na mabadilishano ya wanafunzi, DAAD, litatoa taarifa kuhusu masomo ya juu nchini Ujerumani

Nembo ya taasisi ya Goethe

Nembo ya taasisi ya Goethe

Taasisi ya Goethe jijini Nairobi Kenya leo inafungua milango yake kwa umma kwa lengo la kutoa habari kuhusu shughuli za idara zake tatu, zikiwemo idara ya utamaduni, idara ya maktaba na habari na idara ya lugha ya Kijerumani. Washiriki wengine kwenye shughuli hiyo ya leo ni shirika la Ujerumani linalohusika na mabadilishano ya wanafunzi, DAAD, ambalo litatoa taarifa kuhusu masomo ya juu nchini Ujerumani. Shule ya Kijerumani ya mjini Nairobi na idara ya lugha ya Kijerumani ya chuo kikuu cha Nairobi, pia zitawakilishwa leo katika taasisi ya Goethe.

Josephat Charo alipata fursa ya kuzungumza na msemaji wa taasisi ya Goethe mjini Nairobi, Bi Irene Bibi, ambaye kwanza alikuwa na haya ya kueleza.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

 • Tarehe 18.06.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Nwu5
 • Tarehe 18.06.2010
 • Mwandishi Josephat Nyiro Charo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Nwu5
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com